IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA HATA KIDOGO

 • Published on
  08-Jan-2017

 • View
  41

 • Download
  2

Transcript

 • IKULU SI MAHALA PA KUKIMBILIA! NI MAHALA PATAKATIFU; IKULU NI MZIGO; MSITEMEE MATE KABURI

  LANGU- Mwal J.K NYERERE (AHERA) Rai ya Mtanzania

  Na: Prof Handley Mpoki Mafwenga

  Ph.D (finance -COU), MSc (finance -Strathclyde), MBA (Mg.Eco -ESAMI/MsM), LLM (taxation- UDSM), LLB (Tudarco), PGD tax mgt (IFM), AD tax mgt (IFM)]

  Usiku nalala ghafla usingizi mzito unanipata; Mara namuona Muasisi wa Taifa

  hili baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ananipa barua

  niwaletee watanzania na kuniagiza wasilitemee mate kaburi langu kwa kivuli

  cha Katiba na Madaraka ya Urais. Anaeleza jinsi ambavyo alinusurika kupata

  kifo kwa kile alichoita Adha ya Uhaini ya Mwaka 1964 na 1982 kama

  ifuatavyo.

  Mnamo tarehe 20 Januari, 1964, nilikoswa kupinduliwa na Jeshi la Tanganyika

  Rifles ambalo liliasi na Maasi hayo yalizimwa tarehe 25 Januari, 1964. Maasi

  yalihusisha Vikosi vya Dar-es-salaam na Tabora Brigedi ya Kwanza na ya Pili.

  Kipindi hiki ndicho kipindi cha Majeshi ya Ukombozi ya Msumbiji pia

  yalipambana katika nchi yao.

  Ilipofika Saa 7.50 alfajiri, ya tarehe 21 Januari, 1964, Mkuu wa Kikosi cha

  Kwanza cha TR Brigedia Patrick Sholto Douglas, aliamshwa nyumbani kwake

  na Sauti ya Baruji na Vingora, karibu na Kambi ya Jeshi la Colito ambayo sasa

  inaitwa Lugalo Barracks. Alipotoka nje, aliona askari wake 12 wameshikiliwa

  na wenzao wenye silaha na hatimaye kutiwa Mahabusu. Ndipo alipofahamu

  kwamba, baadhi ya Askari wa Kikosi hicho walikuwa wameasi. Aliweza

  kutoroka yeye na familia yake hadi katikati ya Jiji, akaiacha familia kwa Balozi

  wa Australia nchini, kisha akakimbilia kwa Afisa mwenzake eneo ya Oysterbay

  Dar-Es-Salaam.

 • Akiwa huko, akampigia simu Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akimuomba

  kupeleka ndege tatu Kikosi cha pili cha huko Tabora, kuleta askari waliokuwa

  bado waaminifu kwa Serikali. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa wamefunga

  barabara iendayo Uwanja wa ndege huko Ukonga; hii ikawalazimu Marubani

  warudi mbio inasemekana Brigedia Patrick Sholto Douglas akakimbilia kwenye

  Ubalozi wa Uingereza, akajificha kwa siku tano hadi tarehe 25 Januari, 1964.

  Brigedia Patrick Sholto Douglas alimpigia simu Mkuu wa Polisi, ambaye

  alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Makamu wa Rais wakati huo Mzee

  Rashid Mfaume Kawawa, na kumwamsha, kisha hao wawili wakaja kunipa

  habari.

  Nilihamaki na kukasirika sana; nikataka kwenda mimi mwenyewe kukutana na

  Waasi hao ili wanieleze sababu za kitendo hicho cha aibu; lakini Honey wangu

  Mama Maria kwa machozi na kwa kupiga magoti, alinisihi nisitoke kwenda

  kukutana na watu wenye silaha. Nilimkaidi mpenzi wangu lakini Juhudi za

  ziada zilifanywa baadaye nilikubali. Radhid Kawawa na Mama Maria Nyerere,

  wakatorokea mahali nisikokujua. Wakati huo, tayari Waasi walikuwa kwenye

  lango kuu la Ikulu wakinitafuta.

  Kufikia saa 9.00 alfajiri siku hiyo hiyo, Waasi walikuwa wamekamata Kambi

  ya Colito (Lugalo), kisha wakajigawa Vikundi vitatu na kuingia mjini. Kikundi

  kimoja kilibakia kulinda Kambi hiyo, Kikundi cha Pili, kikiongozwa na Sajini

  Francis Higo Ilogi, ndicho kilichokuja Ikulu kunitafuta, wakati Kikundi cha tatu

  kililinda barabara kuu zote mjini.

  Kikundi cha Sajini Ilogi kilipofika Ikulu, kiliruhusiwa na Mmoja wa Maafisa

  Usalama wa Taifa, wamuone kwanza Waziri Mheshimiwa Oscar Kambona; nao

  wakakubali kufanya hivyo. Wakaenda hadi kwa Kambona na kumleta Ikulu, na

  kumweleza kwamba walikuwa wamewakamata na kuwaweka Mahabusu baadhi

  ya Wanajeshi ambao wanasemekana walikuwa 16; na kwamba, kama

  Mheshimiwa Oscar Kambona alikuwa tayari kusikiliza Malalamiko yao,

  afuatane nao hadi Colito (Lugalo). Kamabona alikubali, aliondoka akiwa

  amepanda gari la Mkuu wa Polisi na aliweza kukubali kuandamana na askari

  wenye silaha, na wenye hasira kali kwenda Colito Barracks.

  Walipofika Colito Barracks, walimtaka Oscar Kambona aaamue papo hapo,

  pamoja na mambo mengine kuondolewa mara moja kwa Maafisa wa Kiingereza

  Jeshini, na nafasi zao zishikwe na Wazalendo. Walitaka pia mishahara

  iongezwe, kutoa Shilingi za Tanzania 105/= hadi kufikia Shilingi za Tanzania

 • 260/= kwa mwezi. Hata hivyo, Mheshimiwa Oscar Kambona aliomba wateue

  wawakilishi wachache ili wafuatane naye hadi Ikulu kwa Mashauriano nami

  (Nyerere). Ndipo Kiongozi wa Waasi hao Sajini Francis Higo Ilogi, alipokataa

  na kusema Tunataka kila kitu leo hii Yowe zikasikika Apigwe risasi,

  apigwe Kambona huyo. Kwa kuogopa kuuawa, Kambona akauliza, Mnataka

  nani awaongoze? Lilitajwa jina la Alex Nyirenda; lakini likakataliwa kwamba

  alikuwa na majivuno. Akatajwa Luteni Elisha Kavana, akapitishwa kwa kauli

  moja na kuvishwa kofia ya Brigedia Douglas.

  Walipofika huko, askari hao walijipanga barabara iingiayo Ikulu, ingawa Sajini

  Ilogi aliwakataza wasiingie ndani; Baada ya mashauriano kwa muda na

  wasaidizi wa Rais pamoja na Mama mzazi wa Mwalimu Nyerere, Kambona

  alitoka nje na kuwatangazia Waasi hao kuwa Rais ameyakubali madai yao;

  Lakini askari hao wakapiga kelele Muongo huyo Rais hayumo ndani; mpige

  risasi, muongo huyo Hata hivyo, waliondoka wameridhika, wakarejea

  Kambini siku hiyo. Hima, Kambona aliwaondoa Maafisa wa Uingereza na

  kuwasafirisha kwao kupitia Nairobi Kenya.

  Akiwatangazia Wananchi kupitia Kituo cha Redio wakati huo Tanganyika

  Broadcasting Corporation (TBC), Mzee Oscar Kambona alisema;

  Huyu ni Waziri wenu wa Mambo ya Nje na Ulinzi; Serikali

  ingalipokumekuwa na kutoelewana baina ya askari Waafrika na Maafisa

  wa Uingereza katika Jeshi. Baada ya kuingilia kati Shauri hili, sasa askari

  wamerudi kambini

  Kuna uwezekano mkubwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi

  Mheshimiwa Oscar Kamabona ndiye aliyewashawishi Wanajeshi walioasi

  Januari, 21, 1964 kurejea Kambini, kwa ahadi ya kushughulikia malalamiko

  yao; siku ya pili baada ya kurejea Kambini, askari Waasi walionekana kufurahi

  baada ya Maafisa wa Uingereza kuanza kuondoka, kama walivyoahidiwa na

  Oscar Kambona. Ingawa, Sajini Francis Higo Ilogi hakuwa na furaha kama

  wengine.

  Nakumbuka, wakati wa Uasi Mwarabu mmoja alifanikiwa kuwaua Askari

  wawili mtaani ambao walizikwa Dar-Es-Salaam. Wakati wa maziko ya askari

  hao, ilipokelewa taarifa kwamba, Kikosi cha pili cha Jeshi kilichokuwa Tabora

  nacho kilikuwa kimeasi, baada ya kupata habari kwamba wenzao wa Colito

  {Lugalo} walikuwa wameasi.

 • Wakati Kikosi cha Tabora kikiendelea na Maasi, ilipokelewa hapo Tabora simu

  ya maandishi (Telegraph) kutoka kwa Mhehimiwa Oscar Kambona kuwa

  Kapteni Mirisho Sam Hagai Sarakikya, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha

  Tabora. Wakati huo Sarakikya na Maafisa wengine walikuwa wamekamatwa na

  kuwekwa Mahabusu na askari walioasi hapo Tabora.

  Ndugu yangu Sarakikya akatolewa Mahabusu na akaomba simu hiyo isomwe

  kwa sauti; kisha akatoa amri wasimame Mguu Sawa, wafunge beneti na kutoa

  risasi. Nao wakamtii. Usiku huo, Sarakikya alifanya Mipango ya kuwasafirisha

  maafisa wa Uingereza kutoka Tabora kwenda Dar-Es-Salaam na hatimaye

  Makwao.

  Tukio la Januari, 21 1964 na lile la Tabora pamoja ilienda sambamba na hali ya

  Hatari huko Kenya, Uganda na Zanzibar, ambapo Serikali ya Uingereza ilibidi

  ichukue tahadhari ya ziada kwa kupeleka askari wanaokisiwa kuwa 2,000 ndani

  ya Ukanda wa Afrika ya Mashariki. Kwa hiyo, Manowari iliyoitwa Rhy, ikwa

  imetia nanga hima Pwani ya Dar-es-salaam, na nyingine iitwayo Centaur,

  iliyobeba ndege iliwasili na askari wapatao kama 600.

  Nilifanya mazungumzo na Waasi; lakini ilipofika Ijumaa ya tarehe 25

  Mazungumzo hayo hayakufikiwa vyema kwani Viongozi wa Vyama vya

  Wafanyakazi, kupitia Chama Kikuu (Shirikisho) cha Wafanyakazi

  (TFL),walikuwa wakikutana kwa siri na askari walioasi kwenye Kambi ya

  Colito (Bienne P43); na Vyma hivyo vilikuwa vimeandaa Mgomo nchi nzima

  kuungana na askari hao. Ilipofika saa 11.30 jioni siku hiyo, nilimuita Ikulu

  Naibu Balozi wa Uingereza Bwana F. Stephen Mills; kumuomba Msaada wa

  Kijeshi wa nchi yake na Mills bila kuchelewa, akapeleka taarifa London na

  maombi kukubaliwa bila masharti yoyote.

  Wakati huohuo, Mheshimiwa Oscar Satiel Kambona, akaenda mbio kwenye

  Ubalozi wa Uingereza kumtafuta Brigedia Douglas ambaye alikuwa amejificha

  humo kwa wiki nzima, kumuomba msaada wa kuratibu Mipango. Usiku wa

  siku hiyo, Douglas na Ofisa mwingine, walinyatia hadi kwenye Manowari

  Centaur iliyokuwa imefichwa.

  Jumamosi ya Januari tarehe 26, 1964 saa 12.20 asubuhi, helikopta sita kutoka

  Manowari Centaur zilichukua askari wanaokisiwa kuwa 60 akiwamo Brigedia

  Douglas hadi eneo la Karibu na Kambi ya Colito. Dakika kumi baadaye saa

  12.30 Manowari hiyo, na meli nyingine ya Vita Cambrian iliyokuwa ikisubiri

  zilianza Mashambulizi kwa kupiga Mizinga kuwatisha Waasi. Wakati huo

 • mpango wa kuwalevya kwa ushindi wao bandia ulifanywa kwa kuchukuwa

  pombe kwenye kiwanda cha Bia cha Ilala na Waasi hao wakanywa ipasavyo na

  ndiyo msingi wa Colito kuitwa Lugalo ikiwa na maana ya pahali pa kulewea

  pombe au tafrija ya pombe kwa lugha ya Kihehe au Kinyakyusa na baadhi ya

  makabila yenye asili ya Kibantu. Kutoka umbari upatao kama mita 20 hivi, na

  kwa ujasiri mkubwa, Douglas akatangaza kwa kipaza sauti, kwamba alikuwa

  ameshika madaraka yake tena; akatoa amri askari wote watoke nje Kambini

  Mikono juu na kukaa chini barabarani.

  Baada ya dakika kumi bila kuona kitu, Brigedia Douglas akaanza kuhesabu

  Moja ; Mbili; Kumi, askari wa Uingereza wakafyatua roketi hadi

  Kambini. Waasi wakaanza kujisalimisha. Dakika kumi zingine zilizofuata

  askari 150 walijisalimisha na wengine 150 baada ya saa moja. Kufikia saa 1.30

  asubuhi, wote walikuwa wamesalimu amri; Maasi yakawa yamezimwa katika

  zoezi ambalo askari walioasi, baadhi waliuawa na wengine walijeruhiwa.

  Nakubaliana, na maoni ya Balozi Abbas Kleist Sykes akinukuliwa kuwa, Maasi

  ya Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) Mwaka 1964 yalitokana na sehemu kubwa

  kwa kuchelewa kuwaondoa Makamanda wa Kizungu na kuwapandisha vyeo

  Waafrika. Kama ilivyofanyika kwa Jeshi la Polisi na Watumishi wengine

  Serikalini. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Maasi ya Kenya na Uganda.

  Kutokana na Maasi hayo, nilikifuta Kikosi chote cha Kwanza (Colito Barracks)

  na kuwafukuza kazi askari 100 wa Kikosi cha Pili cha Tabora. Nilifukuza pia

  asilimia 10 ya askari wa Polisi na Usalama 5,000 waliokuwapo, kwa kushindwa

  kutekeleza Wajibu wao wa Kudhibiti Maasi. Watu zaidi ya 400 walikamatwa na

  kuhojiwa, wakiwamo viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi; na wengine 500

  walitiwa nguvuni chini ya Sheria ya The Preventive and Detention Act lakini

  wengi waliachiwa.

  Nalo lililokuwa Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TFL), lilifutwa, badala yake

  kikaundwa Chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kama

  Jumuiya ya Chama tawaa TANU. Nilimteua Mirisho Sam Hagai Sarakikya

  kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi na kumpandisha cheo kuwa Brigedia.

  Mwanzoni mwa Aprili, 1964, Majeshi ya Uingereza yaliondoka na nafasi yake

  kuchukuliwa na Kikosi cha Tatu cha Jeshi la Nigeria, chini ya Luteni Kanali

  James Pam. Sajini Francis Higo Ilogi alipatikana na Hatia ya Uasi wa Jeshi na

  kufungwa miaka 15, ambapo washirika wake 13 wakafungwa kifungo cha kati

  ya miaka mitano hadi kumi.

 • Jeshi la Tanganyika Rifles (TR) liliundwa baada ya Tanganyika kupata Uhuru

  tarehe 9 Desemba, 1961 likibadilishwa kutoka Jeshi la Kings African Rifles

  (KAR) lililokuwa chini ya Waingereza. Pamoja na kubadilika Jina Tanganyika

  Rifles ilikuwa na Muundo sawa na KAR. Jeshi hilo liliongozwa na Jenerali

  Morisho Sarakikya kuanzia tarehe 8 Januari, 1964 hadi tarehe 12 Februari, 1974

  lilipoongozwa na Jenerali Abdalah Twalipo hadi tarehe 8 Novemba, 1980.

  Kipindi Jeshi linaasi, Sheria ya Kuwekwa Kizuizini ilikuwa tayari

  imekwishaundwa yaani Tangayika Preventive and Detention Act, Cap 490 ya

  Mwaka, 1962 kwa sasa ni Cap 361 [R.E 2002]. Hata hivyo, sikuipenda sana

  Sheria hiyo ingawa niliweka saini. Kwa sababu niliamini niSheria

  inayomuweka mtu hatiani bila Mashitaka hali anapaswa kuwa na Haki ya

  kusikilizwa.

  Ukweli ni kuwa nilipata kusema maneno yafuatayo Take the question of

  detention without trial. This is a desperately serious matter. It means that you

  are imprisoning a man when he has not broken any written law, or when you

  cannot be sure of proving beyong reasonable doubt that he has done. You are

  restricting his liberty, and making him suffer materially and spiritually, for

  what you belive he has done. Few things are more dangerous to the freedom of

  a society than that. For freedom is indivisible, and with such an opportunity

  open to the Government of the day, the freedom of every citizen is reduced; to

  suspend Rule of Law under any circumtances is to leave open the possibility of

  the grossest injustices being perpetrated. Yes knowing these things. I have still

  supported the introduction of a law which gives the Government power to

  detain people without trial. I have myself signed Detention Orders. I have done

  these things as an inevitable part of my responsibilities as President of the

  Republic

  Pamoja na Sheria hiyo kuwepo, Mheshimiwa Kasanga Tumbo aliyekuwa

  Kiongozi wa Chama cha Peoples Democratic Party ndani ya Bunge ambaye pia

  aliwahi kuwekwa Kizuizini kuanzia Januari, 1964 hadi Julai, 1966 aliipinga

  vikali Sheria hiyo, iliyotangaza pamoja na mambo mengine Hali ya Hatari kwa

  Watu wa Tanganyika Hata hivyo, niliamini kuwa Sheria hiyo iliwalenga

  wahaini.

  Ilipofika Mwezi Aprili, 1965 raia 14 wa Tanzania mbali ya Wajumbe wa awali

  wa Baraza huko Zanzibar na Wanajeshi wapatao 20 wa Jeshi la Tanganyika

  Rifles waliwekwa Kizuizini. Hata hivyo, ilipofika tarehe 25 Julai, 1966

 • ilitangazwa kuwa Watanzania waliokamatwa kwa ajili ya Uhaini walikuwa

  wameachiwa huru; Hayo yalisemwa na Mheshimiwa Job Lusinde wakati huo

  akiwa Waziri wangu wa Mambo ya Ndani ambaye alisisitiza kuwa kwa mujibu

  wa Sera ya Jumla iliyofikiwa waliotuhumiwa wote wako huru na kuwa kamwe

  haiashirii kuhatarisha Amani nchini.

  Mnamo Mwezi Agosti, 1967, Ndugu Abdalah Khasim Hanga aliyekuwa

  Makamu wa Rais wa Zanzibar, na Mlinzi wake Ndugu Eli Anangisye Mbunge

  wa Tanzania Bara, ndugu zake Oscar Kambona na Maafisa watatu wa Wizara

  ya Mambo ya Nchi za Nje waliohisiwa kuwa mahasimu wa karibu wa Kambona

  waliwekwa ndani kwa kuhusishwa na kufanya njama za Mapinduzi; Hii

  ilijumuisha pia kuwaweka ndani baadhi ya viongozi, marafiki na ndugu.

  Baadaye, ikatangazwa kuwa viongozi wa tuhuma za Mapinduzi hayo

  watafungwa kwa kosa la Uhaini.

  Mbali ya Uhaini huo, pia Nusra nipoteze nafasi ya Urais wa Jamhuri ya

  Muungano wa Tanzania, mnamo Mwaka 1982. Jaribio hilo la Mapinduzi

  lilifanywa na baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania wakisaidiana

  na Bwana mmoja aliyeitwa Thomas Pius Mtakubwa Rugangira huyu alijulikana

  pia kwa majina ya Father Tom au Unle Tom.

  Kipindi hicho idara yangu ya Usalama ilitumia sana usafiri wa Teksi na hata

  bendi maarufu ya DDC Mlimani park msingi wake mkubwa ni chama cha

  Tanzania Transport, Tax and Services (TTTS) kilikuwa na watu wenye weledi

  huo. Hivyo, Watuhumiwa hao walifichuliwa njama zao na dereva teksi mmoja

  waliyekuwa wakimtumia mara kwa mara ambapo njama zao zilikuwa kuniua na

  kuniondoa Madarakani na Kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa

  Tanzania. Hivyo walikabiliwa pia na Shitaka mbadala la kuficha kosa la Uhaini

  kwa kushindwa kutoa taarifa kwa Mamlaka iliyohusika huku wakielewa juu ya

  Mpango wa Kuipindua Serikali.

  Sikupenda sana iwepo kesi dhidi yao kwani nikiwa Mkatoliki niliyekuwa

  kwenye Jumuiya Parokia ya Msasani na hata Kanisa la Mtakatifu Petro la

  Oysterbay nilijifunza kusamehe mara saba sabini. Lakini Dola iliamua Kesi ya

  Uhaini iungurume hapa nchini Tanzania chini ya Mheshimiwa Jaji Nassor

  Mnzavas. Washitakiwa kwenye kesi hiyo walikuwa 19; miongoni mwao

  alikuwepo Thomas Rugangira au Uncle TOMau Father Uncle Chek Bob,

  wenzake walikuwa ni Khatibu Ghandhi au Hatty MacGhee, Kapteni

  Mohammed Tamimu, Kapteni Ditrick Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege,

 • Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Vitalis Mapunda. Wengine

  walikuwa ni Banyikwa na Mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Has Pope,

  Kapteni Rodrick Rosham Robert na wengine ambao jumla yao walikuwa 19.

  Kundi hilo lilikuwa na vijana watundu waliojiita Makomandoo sikumbuki

  walijifunza wapi? Ambao ni Rugangira na Hatty MacGhee ambao wakati Kesi

  inaendelea walipanga njama na kufanikiwa kutoroka katika Gereza la Keko,

  Mjini Dar-Es-Salaam.

  Vijana wale walitorokea nchini Kenya na baada ya kufika Kenya, Rugangira

  akatorokea nchini Uingereza. Wakati huo viwanja vyetu vya ndege havikuwa na

  ulinzi sana na hata mipakani hapakuwa na ulinzi mkali kubaini utorokaji wao.

  Kwa bahati nzuri, Yule kijana Hatty MacGhee tukafanikiwa kumkamata na

  kumrudisha hapa Tanzania; kukawa na Makubaliano na Kenya ya

  kubadilishana wahalifu na ndipo tukabadilishana na mtu mmoja aliyekuwa

  akitakiwa Kenya aliyetajwa kwa jina la Private Hezekiah Ochuka ambaye

  ilidaiwa kuwa alifanya madudu huko Kenya.

  Kijana Hatty MacGhee aliporejeshwa nchini aliunganishwa na wenzake na kesi

  ikapamba moto. Nakumbuka, Katika Jaribio hilo, Komandoo Tamimu aliuawa

  wakati wa purukushani za kumkamata pale Kinondoni Mkwajuni Dar-Es-

  Salaam wakati wakimkimbiza Komandoo Tamimu alidandia gari moja Pick Up

  iliyokuwa imebeba masanduku ya bia na kuanza kuwarushia wanaUsalama

  waliokuwa wakimkimbiza, hivyo akapigwa risasi na kufa.

  Ingawa nakumbuka, Mahakamani wakati wa kutoa ushahidi juu ya Komandoo

  huyo mwanaUsalama mmoja aliyekuwa akiitwa MrX alisema walijaribu

  kumkamata lakini akawatoroka kwa kuruka ukuta wa nyumba aliyokuwa

  akiishi.

  Kesi hiyo ya Uhaini ilikuwa imesimamiwa na Wakili machachari wa Utetezi

  aliyejulikana kwa jina la Murtaza Lakha mwenye asili ya Asia. Mawakili

  wengine wa Utetezi alikuwepo Mucadam, Jadeja na Tarimo. Upande wa

  Serikali ulikuwa unaongozwa na Wakili William Sekule, pia alikuwepo Johnson

  Mwanyika.

  Watuhumiwa wengine sita wa Uhaini waliachiwa huru siku mbili baadaye

  kutoka kwenye Gereza la Ukonga Dar-Es-Salaam. Wakati wakiachiwa huru,

  Maganga alikuwa amehamishwa kwenye Magereza mengi ndani ya Dar-Es-

 • Salaam na Gereza lake la mwisho lilikuwa Butimba Mwanza. Pamoja na tabu

  walizozipata Gerezani Eugen Maganga anadaiwa kusema;

  Hatujutii kujaribu kuangusha Serikali bali tunajutia tu kwa kushindwa kwa

  Mipango ya kupindua.

  Kabla hawajafikia kuwa na wazo la kuangusha Serikali, Maganga aliyekuwa na

  miaka 26 na Kadego walifika Jeshini na Tank Battalion. Maganga alikuwa

  Luteni wakati Kadego alikuwa Kapteni.

  Maganga alikuwa ndiyo anarudi kutoka Mjini London Uingereza ambapo

  alikuwa akipata mafunzo ya kujinoa Kijeshi ya kupigana vita ya Uganda

  Mwaka 1978. Akiwa mmoja wapo ya askari wa mstari wa mbele, Maganga

  anaamini Tanzania ilishinda vita dhidi ya Uganda kwa vile Uganda ilikuwa na

  Jeshi dhaifu.

  Moja ya sababu walizozibainisha ni pamoja na 1) kutokuwa na furaha jinsi

  Watanzania walivyokuwa Maskini na kulazimishwa kwenye Vijiji vya Ujamaa ;

  2) Vita dhidi ya Uganda na Tanzania havikuwa na umuhimu na hivyo kuishia

  kutumia fedha vibaya-vita havikuwa vya nchi hizi mbili bali vita vya Mwalimu

  Julius Nyerere na Idd Amin na pia 3) Hali iliyokuwepo Jeshini ilikuwa siyo

  nzuri ukilinganisha na hali iliyokuwepo wakati wa Meja Jenerali Mrisho

  Sarakikya, Kiongozi wa Kwanza wa Jeshi la Ulinzi toka Mwaka 1964 hadi

  1974 4) Waliopanga njama za kuangusha Serikali walihisi kuwa mimi

  (Nyerere) sina imani na watu wa Kaskazini kwa sababu wamesoma nje ya nchi

  na hivyo nawahofia kuwa wanaweza kuangusha Serikali 5) Watu waliokuwa

  hawajasoma sana ndiyo waliopewa Madaraka na kuwa mambo hayakwenda

  sawa; na 6) Wanajeshi hawakupewa vyeo na kuwa mimi nilipenda kujenga

  Jeshi lenye watu ambao hawawezi kunipa Changamoto zozote.

  Wahaini hao walidhani wangefanya mabadiliko bali inaonekana watu ambao

  walijipanga nao hawakuwa tayari kujitoa Mhanga. Hata hivyo, hawakukata

  tamaa, wakiwa baadhi yao wanapanga njama hizo wakakutana na Marehemu

  Thoma Pius Rugangira ambaye alikuwa Mfanyabiashara wa Tanzania huko

  nchini Kenya, na alikuwa akiishi pia Uganda na kwa vile baba yake Mzazi

  alikuwa Uganda alikuwa akidhaniwa kuwa ni Afisa Usalama wa Serikali ya

  Uganda.

  Wahaini hao hawakuwashirikisha kabisa viongozi wa juu wa Jeshi waliweza

  kujipanga wenyewe wakiwa vijana wadogo. Thomas Pius Rugangira ndiye

 • alikuwa mfadhiri wao na kamwe hawakupata fedha zozote nyingi toka nje ya

  nchi. Wahaini hao walidhani wangeweza kuleta mfumo wa Demokrasia ya

  Vyama Vingi ambako watu huwa huru kutoa mawazo yao na kuchagua Rais wa

  nchi wanayemtaka. Waliahidiwa kuwa Thomas Pius Rugangira ndiye ambaye

  angechukua nafasi ya Uwaziri Mkuu badala ya kuwa na mimi (Nyerere) kwa

  masharti kuwa asingepaswa kugombea nafasi ya Urais kwa muda wa Miaka

  iliyokuwa inafuata.

  Siku tatu kabla ya Uhaini kufanyika Thoms Pius Rugangira aliwauliza ni nafasi

  gani wangehitaji kama wakiunda Serikali mpya; lakini walijibu kuwa

  wasingehitaji chochote.

  Wakati Mipango yote imekuwa tayari, walisubiri nirudi toka nje ya nchi kwani

  nilisafiri; Nilirudi Mnamo Mwezi Januari, 1982 baada ya kukaa nje kwa muda

  wa miezi miwili na kwenda nyumbani kwetu Butiama. Lengo lao la kunisubiri

  ilikuwa kuniuwa na mipango hiyo ilipendekezwa na Thomas Pius Rugangira.

  Bila matarajio, nilikaa muda kidogo pale Butiama na sikurudi Dar-Es-Salaam

  katika kipindi cha siku mbili ambazo Mapinduzi yalipangwa ambapo

  yalipangwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 9 Januari, 1982. Siku ya Ijumaa

  Mnamo tarehe 6 Januari, 1982 wakapanga kukutana kwa mara ya mwisho kabla

  ya kutekeleza Uhaini wao; hata hivyo, baadhi ya wenzao hawakuonekana.

  Mohammed Tamimu ni mmoja ya Wahaini ambao hawakuonekana siku hiyo.

  Wajumbe wengine walihofu sana kitendo cha Mohammed Tamimu

  kutoonekana. Wakaamua kumtuma mmoja wao Kinondoni Mkwajuni ambako

  alikuwa anakaa, lakini wakashangaa kuona Polisi wamezingira nyumba yake na

  wamemuuwa. Hapo wakagundua kuwa suala lao siyo siri tena. Mohammed

  Tamimu alikuwa na kawaida ya kutunza rekodi za mikutano yao na majina ya

  wahusika.

  Ikawa Polisi na Wanausalama wameanza kuwasaka; Kadego na Maganga

  wakaamua kutorokea Kenya kupitia Tanga na Mombasa ambapo walikaa

  Nairobi miezi kumi kama Wakimbizi wa kisiasa. Hawakujilaumu sana kuvuja

  kwa Suala lao kwani waliamini pengine Hatty MacGhee ametoa siri kwa vile

  alikuwa raia na alikuwa hajui kutunza siri. Walihisi pia kuwa Mohammed

  Tamimu alijua kuwa Hatty MacGhee hakuwa Askari Mstaafu wa Jeshi la

  Marekani kama alivyojitapa na wakagundua baadaye kuwa jina lake halisi

  alikuwa Khatibu Hassan Ghandhi na alikuwa rubani Mtanzania.

 • Kuna wakati siku chache baadaye, Maganga na Kadego wakiwa wanazurura

  mitaa ya Nairobi ghafla wakawaona Wahaini wenzao Uncle Thom na Hatty

  MacGhee waliokuwa wamewaacha Dar-Es-Salaam. Hawa watuhumiwa wawili

  walikuwa wametoroka katika Gereza la Keko lililopo mjini Dar-Es-Salaam.

  Ingawa walifurahia maisha pale Nairobi, Rugangira aliamua kusafiri kwenda

  London Uingereza kujaribu kutafuta njia ya kuwahamishia Malawi. Alihofu

  kuwa Serikali ya Kenya ingeshirikiana na Serikali ya Tanzania kuwakamata.

  Watuhumiwa wa Uhaini wote nane, walifanikiwa kutorokea Nairobi. Kabla ya

  Pius Rugangira hajarudi kutoka London kundi lao likakamatwa Nairobi na

  wakabadilishana na Koplo Ochuka na Sajini Pancras Oteyo ambao nao

  walikuwa na Mpango kama huo wa kuagusha Serikali ya Rais Daniel Arap Moi

  wa Kenya Mwaka huo huo wa 1982 na wakakimbilia Tanzania. Walifungwa

  pingu mikononi na kufungwa vitambaa usoni na kupelekwa kwenye Gereza la

  Isaka lenye ulinzi Mkali lililopo Mjini Dodoma ambako walikaa kuanzia Mwezi

  Novenber, 1983 hadi Oktoba, 1084.

  Watu waliokuwa wanawalinda hawakuwa wakali sana, kitu kilichowafanya

  waweze kuandika barua Ubalozi wa Marekani wakitaka Dunia ielewe kuwa

  walifungwa kwa sababu hakuna mtu alikuwa anajua chochote wakati huo. Hii

  ilifanya Kamishana wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa kutembelea Tanzania

  na kulazimisha kupeleka Kesi Mahakamani.

  Kesi ilianza kuunguruma rasmi Januari, 1985 na Mnamo tarehe 28 Desemba,

  1985 Mheshimiwa Jaji Nassoro Mnzavas alitoa Hukumu ambapo washitakiwa

  wengine aliwafunga kifungo cha maisha na wengine walifungwa miaka kadhaa

  lakini Banyikwa na Ngaiza waliachiwa huru.

  Kwenye Gereza la Butimba, ndipo alipokuwepo Eugene Maganga ambapo

  Mnamo tarehe 22 Oktoba, 1995, Rais Ali Hassan Mwinyi alitoa Msamaha na

  wenzaka kadhaa.

  [HAKIKA IKULU SI PA KUKIMBILIA MUNGU IBARIKI AFRIKA

  IBARIKI TANZANIA]